logo

‎LUKUVI KUZIKWA MACHI 31,2026 IDODI MKOANI IRINGA

Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), William Lukuvi (70) utazikwa Kijiji kwao Idodi, Wilaya ya Iringa Vijijini, Jumanne ya Machi 31, 2026.

Lukuvi ambaye pia alikuwa mbunge wa Isimani (CCM) alifariki dunia saa 1 asubuhi ya jana Jumatano, Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu ya mshtuko wa moyo.

‎Leo Alhamisi, Machi 26, 2026, ratiba ya mazishi ya Lukuvi imetolewa ikionesha kesho Ijumaa mwili wa Lukuvi utaagwa na wabunge katika viwanja vya Bunge, Dodoma na Jumamosi ya Machi 28, 2026, mwili wake utaagwa jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Karimjee.

‎Jumapili ya Machi 29, 2026, mwili wa Lukuvi utasafirishwa kwa ndege hadi Iringa Mjini na kesho yake ya Machi 30, utaagwa Iringa Mjini eneo la Gangilonga kabla ya siku hiyohiyo kupelekwa kijiji kwao, Idodi, Jimbo la Isimani ambalo aliliongoza kwa miaka 31 kuanzia mwaka 1995.

‎Mazishi ya Lukuvi aliyekuwa mbunge mkongwe kuliko wote bungeni yatahusisha viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Lukuvi ameacha watoto watatu na mjane mmoja.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn