logo

DKT.BITEKO AZINDUA WODI MPYA KATIKA HOSPITALI YA KUMBUKUMBU YA CHARLES KULWA

Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt.Doto Biteko amezindua wodi mpya katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Charles Kulwa iliyoko Runzewe wilayani Bukombe ambapo wodi hiyo ni maalum kwa ajili ya kuhudumia wanawake wajawazito wanaofanyiwa upasuaji.

Akiwa hospitalini hapo, Dkt.Biteko alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo iliyoanzishwa mwaka 1992 ikiwa kama Zahanati, mwaka 2005 ilipanda hadhi ya kuwa Kituo cha Afya na mwaka 2020 ilipandishwa hadhi ya kuwa hospitali ya Wilaya, ambapo aliupongeza uongozi wa hospitali hiyo inayohudumia wagonjwa takribani elfu 72 kwa mwaka.

Awali, akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella ambaye alikuwa mgeni maalum, alimshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya kuinua sekta Afya katika Mkoa wa Geita na maeneo mengine nchini akitolea mfano ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato.

Aliwataka wadau wengine kuiga mfano wa wamiliki wa hospitali hiyo kwa kuhudumia wagonjwa wengi na kutoa huduma kwa kiwango cha hali ya juu hadi kufikia hatua ya kupandishwa hadhi.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn