logo

MWIMBAJI ZAHARA AAGA DUNIA, "KIPAJI KILICHOACHA ALAMA NCHINI SOUTH AFRICA"

Na Zeyner Qassim ✍️

Nimepata kuusikiliza muziki wake mara nyingi,bila hata kujua maana ya alichokiimba, mbali na 'lyrics' zake kuna uzuri wa kipekee wenye kuvutia ndani ya muziki wake...uzuri unaoishi kwa miaka na mikaka.

Bulelwa Mkutukana @zaharasa , Mtunzi na mwimbaji wa muziki wa kiafrika wa Afro Soul, watu wengi walipata kumfahamu zaidi kupitia kibao chake maarufu cha "Loliwe" chenye maana ya "Gari-moshi/treni".

Katika mahojiano na NTV, Zahara alieleza kuwa aliandika wimbo huo ili kumtia moyo yeyote mwenye kuusikiliza aweze kuifikia hatima yake kwa kuwa mvumilivu na mstahimilivu.

Wimbo huo unaihusu treni iliyowasafirisha baba zake na mababu zake kutoka mji wa Johannesburg hadi London Mashariki enzi za kushamiri kwa ubaguzi wa rangi nchini Afrika kusini,

Licha ya nyakati hizo kuwa ngumu kwa kuwalazimu watu kutengana na ndugu na jamaa zao lakini wengi wao walikuwa na matumaini kwamba gari-moshi hilo litawarejesha wapendwa wao.

Wimbo wa 'Loliwe' ambao ulitungwa kwa gitaa la nyuzi tano,umempatia Zahara tuzo mara dufu...ikiwemo tuzo ya msanii bora wa kike chipukizi wa mwaka 2011, katika tuzo za 18 za @thesamas_ wards, ukawa ni wimbo bora ulioongoza kwa mauzo zaidi katika tuzo za @aforementionedproductions ukawa wimbo bora wa mwaka 2011 katika tuzo za Metro FM... na wimbo huo ukamuwezesha kuwania tuzo mbalimbali nchini Afrika kusini.

Amefariki akiwa na umri wa miaka 36 huku chanzo kikidaiwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya ini na alilazwa hospitalini kwa wiki 2 hadi mauti yalipomfika.

Mungu ampumzishe kwa amani Bulelwa Mkutukana, ninaamini muziki wake utabaki kuwa hazina kubwa katika tasnia ya muziki barani Afrika. 🕯

.

#ripzahara #flyinpeace ❤️🕊

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn