logo

JENERALI MKUNDA AONYA ASKARI WAPYA JWTZ DHIDI YA SIASA NA DAWA ZA KULEVYA

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, amefunga rasmi mafunzo ya askari wapya katika hafla iliyofanyika Januari 31, 2026, kwenye viwanja vya Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi (RTS) Kihangaiko, Msata mkoani Pwani.

‎Akizungumza katika hafla hiyo, Jenerali Mkunda amewataka askari waliomaliza mafunzo kuishi kwa kuzingatia kiapo cha utii wakati wote wanapotekeleza majukumu yao katika maeneo mbalimbali watakayopangiwa, akisisitiza kuwa askari watakaokiuka kiapo hicho watachukuliwa hatua za kinidhamu.

‎Ameonya dhidi ya vitendo vinavyokiuka taratibu za kijeshi, ikiwemo kujihusisha na siasa, matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, matumizi ya dawa za kulevya, michezo ya kamari pamoja na kujiingiza kwenye madeni yasiyo na tija.

‎Aidha, amewahimiza askari hao kutunza afya zao kwa kuzingatia lishe bora na kuepuka uhalifu wa aina yoyote, akieleza kuwa vitendo hivyo ni kinyume na sheria na misingi ya Jeshi.

Jenerali Mkunda amesisitiza askari hao kuwa tayari kiakili na kisaikolojia kuitetea nchi kwa uadilifu ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

‎Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi Kihangaiko, Brigedia Jenerali Sijaona Michael Myala, amewapongeza askari waliomaliza mafunzo na kueleza kuwa wameandaliwa kukabiliana na changamoto mbalimbali za ki

usalama.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn