logo

WAZIRI DKT.GWAJIMA: MPANGO WA KUKAMILISHA PROGRAMU YA PJT-MMMAM HALMASHAURI ZOTE 184 UTAFIKIA APRIL,2024

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa rai kwa watekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) kuhakikisha wanatenga bajeti ili kufanikisha malengo ya mpango huo.

Ametoa Rai hiyo wakati akifungua Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa mpango hey sekta zote sambamba na kuzindua Mwongozo Jumuishi wa Taifa wa Utekelezaji wa Mpango huo (PJT-MMMAM) Desemba 11, 2023 jijini Dodoma.

Waziri Dkt.Gwajima amesema, Wizara inatambua umuhimu wa Wadau hao katika utekelezaji wa PJT MMMAM ambapo amewataka kuainisha vipaumbele kwa uratibu wa Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa ili kuingizwa kwenye bajeti ya Serikali ya 2024/25 kwani kwa kufanya hivyo, uwekezaji wa malezi na makuzi ya watoto wa miaka 0-8 utaongezeka.

"Hakikisheni mnafanya kazi kama timu kwa kuratibiana vizuri kwa kuwa malengo ya programu ya MMMAM hayawezi kufikiwa bila kuzishirikisha sekta zote kwa uwiano na umuhimu unaofanana "alisema Dkt.Gwajima.

Aidha ameyahimiza Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuongeza jitihada ya kuwekeza katika program hiyo kwa kushirikiana na Serikali katika ngazi zote na kuwasisitiza Waandishi wa habari Vinara kupitia umoja wao kuendelea kuelimisha jamii kuhusu program ya MMMAM na tija yake kwa watoto.

Amesema katika kipindi cha miaka miwili tangu kuzinduliwa kwa mpango huo, mafanikio yanaonekana katika utekelezaji wake ikiwemo programu kutekelezwa kwenye Halmashauri 70 za Mikoa 10 ya awamu ya kwanza na mpango wa kukamilisha Programu kwa Halmashauri zote 184 utafikiwa Aprili, 2024

Waziri Dkt. Gwajima amewahimiza pia Wadau kushiriki vema katika mkutano wa Wadau wa MMMAM wa Afrika Mashariki utakaofanyika Jijini Dar es Salaam, Machi 2024.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari UTPC Kenneth Simbaya amebainisha kuwa kupitia Klabu hizo pamoja na vinara wanaungana na Wadau na Serikali kutekeleza.

.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Children in Crossfire Bw.Craig Ferla amesema mpaka sasa hivi mikoa yote 26 nchini imezindua programu ya MMMAM, na pia takribani halmashauri 70 na malengo yako kwa mwakani mwezi Machi,2024 kuweza kufikia halmashauri zote Tanzania.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn