logo

KAGAME ATUA NCHINI KWA ZIARA YA SIKU 2

RAIS wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame, awasili nchini kwa Ziara ya Kikazi ya siku mbili tarehe 27 - 28 April, 2023.

.

Kagame na Ujumbe wake amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax (Mb.)

Katika mapokezi hayo Dkt. Tax aliambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu – Zanzibar Mhe.Jamal Kassim Ali, Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Amos Makala, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Balozi wa Rwanda Nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali.

@wizara_mambo_ya_nje_tz

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn