logo

NDUMBARO: MABADILIKO SHERIA YA NDOA CHIMBUKO LAKE MAHAKAMA

WAZIRI Wa Katiba Na Sheria Dkt.Damas Ndumbaro Amesema Suala La Mabadiliko Ya Sheria Ya Ndoa Chimbuko lake Sio Serikali Bali Ni Muhimili Wa Mahakama ambapo Tayari wameshatoa Amri Hiyo.

.

"Tumeshapewa Amri Toka Mwaka 2019, Na Tumeshapeleka Bungeni Na Bunge Wakasema tuchukue Maoni Zaidi Na Tuko Hapa Kwa Ajili Ya Kujadili Maoni Hayo"

Ndumbaro Ameyasema Hayo Leo April 26,2023 Jijini Dodoma Alipokuwa Akifungua Kongamano la Kitaifa la Sheria Ya Ndoa lililofanyika Katika Ukumbi Wa Morena Hotel.

.

Amesema Serikali Haitungi Sheria Wala Serikali haibadilishi Sheria, Mwenye Mamlaka ya kutunga Na Kubadilisha Sheria ni Bunge la Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania hivyo Ameitaka Asasi za Kiserikali Kulielewa Jambo Hilo.

.

Aidha, Ndumbaro Amesema Hivi Karibuni Bunge La Tanzania Limeielekeza Serikali Kufanya Utafiti Wa Sheria Na Makosa Ya Maadili, Kwa Sababu Vitendo Vya Mmomonyoko Wa Maadili vimekuwa vikiongezeka Mara Kwa Mara.

.

Nae Naibu Waziri Wa Wizara Hiyo Mhe. Pauline Gekul Amesema Kile Ambacho walikuwa Wamekiahidi Kwenye Bunge Sio Jambo La Uongo, Wamekuwa Wakiendelea Na Michakato Ili Suala La Mabadiliko Ya Sheria Ya Ndoa liweze Kufikia Hitimisho.

.

Gekul Amesema Lengo Lao Ni Kuwashirikisha Watanzania Ili waweze Kuona ya Kwamba Wao Ni Sehemu ya Mabadiliko ya Sheria Haijalishi Wewe Una Wazo Gani Lakini Wakishirikishwa watakuwa wapo Salama Zaidi.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn