MBUNGE SALIM: WAFUGAJI NA WAKULIMA WOTE NI WATANZANIA UGOMVI WANINI?
Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe.Salim Alaudin Hasham amewahasa wananchi jamii ya wafugaji kuacha tabia ya kulishia wanyama wao kwenye mashamba ya wakulima kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kupelekea uvunjifu wa amani kati ya wao na wakulima.
Mbunge Salim ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chamwene kitongoji cha changamkeni ambao wanajishughulisha na shughuli za ufugaji wa Ngombe na Mbuzi.
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tu tangu wakulima walipolalamika kuwa wafugaji wamekuwa na tabia ya kulisha mazao katika mashamba yao jambo linalopelekea kukosa chakula hivyo kutaka kuanza kuchukua hatua mkononi.
Kwa upande wao wafugaji wamesema watu wanaofanya michezo hiyo ni wale wafugaji wasio na makazi maalum hivyo wanawachafua hata wale wanaofiata sheria hivyo wameahidi kutoa ushirikiano kwa serikali pindi itakapo wabaini wale wafugaji wenye nia ovu.
Mbunge Salim amemaliza kwa kuwaomba kkudumisha amani na upendo ili kuendeleza utamaduni tulioachiwa na waasisi wa Taifa bila kuvuruga amani kwa matukio yasiyo ya kiungwana.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

