MBUNGE CHEREHANI KUJENGA UWANJA WA MPIRA WA KISASA WENYE NYASI BANDIA JIMBONI KWAKE
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Ng.Emmanuel Cherehani amesema hivi karibuni atajenga uwanja wa mpira wa kisasa wenye nyasi bandia kwa kushirikiana na vyama vya ushirika,halmashauri pamoja na wadau wa michezo na tayari kuna hekari 12 ambazo zimetengwa kwaajili ya ujenzi huo.
Akizungumza baada ya kuhitimisha fainali za Chereheni Cup 2023 ambazo zilishirikisha timu 20 za kata 20 za jimbo hilo,amesema vijana wengi kipindi cha kiangazi ambacho ndicho kipindi cha mashindano mengi viwanja huwa havina nyasi na kupelekea wachezaji kupata michubuko na maumivu makali.
Na kuhusu gharama za ujenzi, Cherehani amesema itatumika sehemu ya fedha za mfuko wa jimbo zitakazotumika kujenga fensi,fedha kutoka halmashauri na fedha kutoka vyama vya ushirika ambavyo tayari vimekubali kuchangia ujenzi huo
Uwanja huo utakuwa wa kwanza katika mkoa wa Shinyanga kujengwa kwa nyasi bandia na ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni baada ya kulipa fidia wananchi walioachia eneo hilo.
.
“viongozi wote wa vyama vya ushirika tumekubali kukata shilingi 5 au shilingi 10 kwenye kila mazao yetu ili tupate fedha nyingi za kujenga uwanja wa kisasa katika jimbo la Ushetu”
Aidha, Cherehani amesema anatamani mashindano yajayo ya Chereheni Cup 2024 yafanyike katika viwanja hivyo.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

