logo

HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA KUANZISHA HUDUMA YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATU WAZIMA

Katika kuelekea Maadhimisho ya Miaka nane (8) tangu kuanzishwa kwa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ambapo Kilele chake itakuwa Oktoba 13,2023, Hospitali hiyo imesema inakwenda kuanzisha huduma ya upasuaji wa Moyo kwa watu wazima.

.

"Tunataka tuongeze wigo wa huduma ya upasuaji wa moyo kwa Watu wakubwa, Tatizo la Moyo pia hata watu wazima wanayo. tumekuwa tukiwapa rufaa wagonjwa waende JKICI lakini Sisi pia tumeona tushirikiane na wadau ili kuweza kuzianzisha hizi huduma hapa" amesema.

.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Dkt.Alphonce B. Chandika ameyasema hayo leo Oktoba 10,2023 Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari juu kuelekea Maadhimisho hayo.

.

Amesema tarehe 16 mwezi Oktoba 2023 wanakwenda kuanzisha kambi ya kufanya matibabu ya Moyo kwa kupitia Upasuaji.

.

"Kuna wagonjwa ambao watafanyiwa Upasuaji huo wa Kufungua kifua na kutokufungua Kifua kwahiyo niwaalike wananchi wajue hizi huduma zipo, wajitokeze kwa wingi waje wapate huduma" Amesema Chandika.

.

Chandika amesema ndani ya miaka minane (8) hiyo, Hospitali ya Benjamin Mkapa imefanikiwa kutoa huduma mbalimbali kwa jamii katika jiji la Dodoma, maeneo ya jirani na hata nje ya nchi.

.

"Tumeshaanzisha huduma nyingi kama mnavyofahamu hapa Benjamin Mkapa kama vile Upandikizaji wa Figo tumefanya kwa kiasi kikubwa,Matibabu ya Moyo kwa kufungua kifua na kutokufungua Kifua, matibabu ya Tezi Dume, Upasuaji,Kupasua mawe kwenye mfumo wa mkojo nk.

.

"Niseme Benjamin Mkapa ni kituo pekee hapa nchini ambacho wananchi wanakimbilia, kuna wengine Wanatoka Dar Es Salaam na sehemu zozote za nchi hii na hata Nje ya nchi wanakuja kutafuta huduma" amesema Dkt.Chandika.

.

Aidha,Mkurugenzi Mtendaji huyo ametoa pongezi wa viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa afya Mhe.Ummy Mwalimu kwa kuweza kuhakikisha hospitali hiyo inafanyiwa maboresho Katika kutoa huduma kwa jamii wakati wote.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn