
MWINJUMA AMALIZA MGOGORO SHIRIKISHO LA FILAMU
NAIBU waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Hamis Mwinjuma, (@mwanafa) ametatua mgogoro wa uongozi uliokuwa ukiliandama Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) na kuwataka Wanachama wa Shirikisho hilo wafuate Sheria, Taratibu na Miongozo inayoliongoza Shirikisho hilo.
Mwinjuma ametatua mgogoro huo mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Shirikisho hilo Aprili 22, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo amewataka wafanye uchaguzi wa shirikisho hilo mapema iwezekanavyo ili wapate viongozi wapya watakaoendeleza tasnia ya Filamu nchini
"Serikali imeweka mazingira mazuri ili mfanye kazi zenu vizuri, hatutaki kuona migogoro, tunataka kuona mkitengeneza kazi bora zinaleta ajira na kuleta ushindani ndani na nje ya nchi" Amesisitiza Mhe. Mwinjuma.
Viongozi hao wameishukuru Serikali kwa kumaliza mgogoro uliokuwepo ndani ya shirikisho hilo wakiahidi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuendeleza tasnia ya filamu nchini.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt. Kiagho Kilonzo.
#JordanMediaupdates
Tranding News

Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news