MWAKAGENDA: NAISHUKURU WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII
MBUNGE wa viti Maalum Mhe.Sophia Mwakagenda ameishukuru Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kudhamini pambano la ngumi la Kimataifa lenye lengo la kukusanya taulo za kike 40,000.
Mwakagenda ametoa pongezi hizo Aprili 22, 2023 wakati wa maandalizi ya mwisho ya pambano hilo litakalofanyika kesho Aprili 23, 2023 katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma kati ya Bondia Hassan Mwakinyo na Kuvesa Katembo kutoka Afrika ya Kusini.
"Nikiwa mratibu wa shindano hili la kirafiki naishukuru Wizara hii kwa kujitoa kudhamini kwa sababu ndio yenye dhamana na watoto wa nchi hii wakiwepo wa kike, kuhakikisha wanapata taulo hizo kwa Ustawi wao" alisema Mwakagenda
Kwa upande wake Bondia Hassan Mwakinyo amesema amekubali kufanya pambano hilo kwa sababu anaamini mwanamke anagusa maisha ya kila mwanadamu.
"Kwa pamoja tulifanikishe hili kuwasaidia watoto wa kike wenye changamoto ya taulo za kujihifadhi" alisema Mwakinyo
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesisitiza kwamba kufanya hivyo ni jambo jema na lenye baraka kuwasaidia watoto wa kike kuondokana na changamoto ya taulo za kike hasa maeneo ya vijijini.
"Wote tunaifahamu dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kujali watoto wa kike" amesema Mhe. Rosemary.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

