
WASANII NAMELESS NA WAHU WATIMIZA MIAKA 18 YA NDOA YAO
Wanamuziki maarufu kutoka nchini Kenya, Nameless na Wahu Kagwi Jumapili hii ya leo Septemba 10,2023 wametimiza miaka 18 katika ndoa yao waliyoifunga miaka mingi iliyopita nyuma.
Kwenye mahojiano aliyoyafanya Wahu na kituo kimoja cha redio cha nchini humo, amekiri ya kwamba kutokuwa na uhakika kama ndoa yao ingefika hata miaka 3 au 4 kutokana na misukosuko waliyokutana nayo na pia wote wawili wamejifunza mengi kutokana na uhusiano huo unaochukuliwa kuwa wa muda mrefu zaidi katika historia ya watu maarufu nchini Kenya.
.
"Tumekuwa na viwango vyetu vya chini sana, viwango vyetu vya juu sana na kati yetu. Mojawapo ya somo kubwa ninaloweza kusema, na siwezi kusisitiza zaidi ni; ikiwa ninyi nyote mnajitahidi kuwa toleo bora zaidi la nafsi zenu, inakuwa bora na bora zaidi," Mwimbaji Wahu Alisema.
.
Wasanii Wawili hao walifunga ndoa yao tarehe 10 Septemba 2005, na kwa hivi sasa ni wazazi wa Mabinti Watatu.
#JordanMediaupdates
Tranding News

Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news