logo

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWATAKA WAATHIRIKA WA VVU KUTOACHA KUTUMIA DAWA MPAKA WATAKAPOJULISHWA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amewataka watu wote wanaoishi na maambukizi ya VVU na Baada ya kupima wakakuta hawana Virusi hivyo wasiache kutumia Dawa mpaka pale watakapojulishwa vinginevyo.

.

"Nalisema hili kwa sababu moja, wapo wenzetu walipata maambukizi wakaanza kupata huduma Vizuri kabisa za ARVs na wakafanikiwa kufubahisha walipopima hakuna VVU mwilini, wakaacha ghafla kutumia Dawa kwahiyo vimewaletea hasara" amesema.

.

Majaliwa ameyasema hayo leo Septemba 07,2023 alipokuwa akimwakilisha Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kilele cha mdahalo wa Kitaifa wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU Tanzania (NACOPHA) uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convertion Jijini Dodoma.

.

Amesema licha ya Tafiti kuonyesha kupungua kwa unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya VVU nchini lakini bado matendo ya unyanyapaa na ubaguzi na ukatili wa kijinsia yanaendelea kuwa kikwazo katika kuzifikia na kuzitumia huduma za VVU hasa kwenye Jamii.

.

"Hili kukabiliana na changamoto hizo ni vema tukaendelea kushirikiana katika kuelimisha jamii yetu hususani kwa kutoa elimu shuleni, Ofisini na katika jamii kwa ujumla wake. ni vizuri makundi na wadau wote mkaanda vitendea kazi vya kutolea elimu kwa njia mbalimbali za sinema, machapisho nk" amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa Amesisitiza kila mtu ni vyema akatambua kuwa ana jukumu kubwa la Pamoja la kuuwisha mipango,Sera na ahadi yake katika kuiwezesha nchi kuyatimiza malengo hayo ya mwitikio wa UKIMWI hapa nchini.

.

Aidha,Majaliwa ametoa wito kwa watanzania kujitokeza na kuunga mkono jitihada za kusaidia watu walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevya nchini.

.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe.Jenista Mhagama amesema mwezi Desemba mwaka huu 2023 wanakwenda kuzindua matokea mapya ya utafiti wa VVU, na wanatarajia nguvu Kubwa iliyowekwa kwa hivi sasa, watanzania watakuwa wameamka na wapo tayari na wataendelea kupima VVU kwa hiari.

.

"Tunakuomba Mhe.Waziri Mkuu uendelee kuwa Balozi wa wanaume wote nchini kuendelea kupima VVU kwa hiari" amesema Mhagama.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn