KANISA LAFUNGWA SIKU 30 BAADA YA WATU KUVUNJA TABERNAKULO YA KUHIFADHIA SAKRAMENTI YA EKARISTI TAKATIFU
Jimbo katoliki la Rulenge Ngara limefunga Kanisa la Mtakatifu Bernadetha wa Lurd Parokia ya Nyakato Buzirayombo lililopo wilaya ya Chato mkoani Geita kwa siku 30 kutokana na tukio la watu wasiojulikana kuvunja ukuta kisha kuingia ndani na kuvunja Tebernakulo ya kuhifadhia Sakramenti ya ekaristi takatifu.
Taarifa ya kufungwa kwa kanisa hilo imetolewa na Makamu wa Askofu wa Jimbo hilo Padri Ovan Mwenge Septemba 01, 2023 ambapo taarifa inaeleza kuwa usiku wa kuamkia Septemba 01, 2023, watu wasio julikana walivunja ukuta wa kanisa na kuingia ndani na Kisha kuvunja kifaa cha kuhifadhia sakramenti takatifu (Tabernakulo).
“Kwa kadri ya maelekezo na sheria ya kanisa kanuni ya 1211-1213 na kwa maelezo ya Askofu Severine Niwemugizi kanisa hilo litafungwa kwa siku 30 kuanzia septemba mosi na baada ya maboresho na ukarabati mdogo wa kanisa hilo litabarikiwa na kutakaswa ili liendelee kutumika” imesema taarifa hiyo.
Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa kwa kipindi hicho waumini wa jimbo hilo wamehimizwa kusali na kufunga pamoja na kufanya toba ya malipizi kwa mwenyezi mungu ili abadilishe mioyo ya watu wenye nia ovu kwa mambo matakatifu.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news