MAONESHO YA MADINI YAFUNGUA FURSA KWA WANANCHI
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Don Resources Mukhusin kikulu amesema uwepo wa maonesho ya madini na uwekezaji mkoa wa Lindi umefungua fursa kwa wakazi wa mkoa wa lindi na ukanda wa kusini kwa ujumla wake kwenye sekta ya madini.
Akizungumza kwenye maonyesho ya madini yaliyofanyika mkoani Lindi katika wilaya Ruangwa,Kikulu amesema hatua ya maonyesho hayo mkoani humo itaketa ufanisi mkubwa katika uzalishaji wa madini na hivyo sekta ya madini kuendelea kuchangia katika Pato la Taifa.
"Maonyesho haya yameuheshimisha mkoa wa Lindi ,umefahamika zaidi hasa katika shughuli za madini,kwa hiyo kuanzia sasa tutakuwa na mchango mkubwa katika ukanda wa kusini lakini pia tutakuwa na mchango mkubwa zaidi kwa nchi yetu kwani naamini kwa maonyesho haya wawekezaji wengi watakuja kufanya kazi kwenye sekta hii ya madini."amesema Kikulu
Amesema maonesho hayo yameweza kufungua fursa na kuelekea kutambua na kugundua maeneo muhimu ambayo yanaonyesha yana madini ili shughuli za uzalishaji ziweze kufanyika katika maeneo hayo ambayo yamefanyiwa utafiti.
"Ndugu wanahabari leo hii tupo Ruangwa, kipekee tunawashukuru waandaaji wa maonyesho haya tumeweza kukutana na Taasisi ya Uwezeshaji Kiuchumi ambayo imenzishwa hapa Ruangwa."
.
Aidha amesema wao kama kampuni ya kizawa wamepata fursa ya kushiriki katika maonyesho hayo ya kuonyesha kazi wanazozifanya kwenye sekta ya madini.
"Sisi tunafanya kazi ya usambazaji wa vifaa na kufanya tafiti mbalimbali kwenye maeneo ya madini na ushauri ."amesema Kikulu.
.
Kwa mujibu wa Kikulu kazi zinazofanywa na Kampuni yake ni kutambua na kutafuta kampuni au wadau mbalimbali wa kitanzania ili waweze kuwangunisha kwa lengo la kufanya kazi kwa pamoja kupitia umoja huo Ili kutambulika kwa urahisi na kutumia fursa zilizopo katika sekta ya madini.
Kwa upande wake Meneja Rasilimali watu na utawala kutoka kampuni ya Akmenite ambayo inajihusisha na ununuzi wa madini na kuchakata madini
Coletha Mwita amesema lengo lakutembelea maonyesho hayo ya madini kwa lengo lakujitangaza na kutafuta watu ambao watawauzia hayo madini na sisi tutayanunua kwa bei elekezi iliyopangwa na Serikali.
"Tupo hapa kuangalia watu ambao wapo tayari kufanya kazi na sisi ambapo pia tunawasaidia wachimbaji wadogo ambao wanaweza kuchimba wameanza kuchimba lakini hawezi kumaliza ile shughuli pale alipofikia kama atahitaji msaada kwetu tutamsaidia ili aweze kumaliza ile kazi lakini pia tutanunua mzigo wake kwa bei mzuri sana hivyo basi tunawakaribisha wachimbaji wadogo wote waje watuuzie madini yao,"amesema Coletha.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

