logo

JKT YATANGAZA NAFASI YA MAFUNZO YA KUJITOLEA KWA MWAKA 2023

JESHI la Kujenga Taifa(JKT)limetangaza nafasi za kujitolea kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mwaka 2023, vijana wote kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wenye sifa za kujiunga na Jeshi hilo huku watakaopata nafasi hizo wametakiwa kuripoti katika kambi za JKT kuanzia Septemba 26 hadi 29 Mwaka huu.

.

Akizungumza leo Agosti 25,2023 na waandishi wa habari Makao Makuu ya JKT Chamwino Mkoani Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa JKT,Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema usaili utaanza Agosti 28, mwaka huu kupitia Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar.

.

“Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele anawakaribisha vijana wote watakaopata fursa kuja kujiunga ili kujengewa uzalendo, Umoja wa kitaifa, Ukakamavu, kufundishwa stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa lao” amesema Brigedia Jenerali Mabena.

.

Amesema utaratibu wa vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo unaratibiwa na ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya ambapo mwombaji anatoka.

Ameongeza kuwa “Vijana watakaochaguliwa watatakiwa kuripoti kwenye nakambi ya JKT kuanzia Septemba 26 hadi 29, 2023, aidha JKT linapenda kuwaarifu Vijana watakaopata fulsa hiyo kuwa halitoi ajira, wala kuwatafutia ajira kwenye asasi, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali au vyombo vya ulinzi na Usalama” amesema.

.

Aidha, amesisitiza kuwa nafasi hizo haziuzwi na waombaji wasirubuniwe na mtu yeyote kwa kumpa fedha ili kufanikisha yeye kupata nafasi za kujiunga na JKT.

“Kumekuwa na wimbi la utapeli unaoendeshwa na baadhi ya watu ambao wakiwaomba fedha vijana wanaoomba nafasi hizo,naomba niwaambie nafasi hizi haziuzwi ni bure hivyo kila mmoja aombe sehemu husika zilizotolewa na JKT,” amesema Brigedia Jenerali Mabena.

Sifa za muombaji na maelekezo ya vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo vinapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn