logo

WATATU WAHUKUMIWA KIFUNGO JELA KWA KUBAKA

MAHAKAMA mkoani Manyara imewahukumu Watu watatu kifungo jela kwa kosa la kubaka.

Waliohukumiwa ni Isaya Mtinanga mkazi wa Gendi Mkoa wa Manyara wilayani Babati amehukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kumbaka msichana wa miaka 15, hukumu iyo imetolewa na Hakimu Mh Kimaro SRM.

Abdallah Mohamed miaka 30 amekuhumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la nne mwenye miaka 12 wa shule ya msingi Babati wilayani Babati, hukumu hiyo imetolewa tarehe 20.04.2023 na Hakimu Mwambago SRM.

Katika shauri Jingine Shedrack Juma (22) mkazi wa Magugu tarehe 20.04.2023 amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kumbaka mwanamke wa miaka 75 tarehe 7/11/2022 huko katika kitongoji Msikiti Kata ya Magugu, Tarafa ya Mbugwe wilayani Babati hukumu iyo imetolewa na Hakimu Mwambago SRM.

.

Kuhukumiwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na upelelezi uliofanywa na Jeshi la Polisi.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn