RAIS WA INDONESIA JOKO WIDODO KUANZA ZIARA YA KITAIFA LEO NCHINI
Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mheshimiwa.Joko Widodo anatarajia kuanzia ziara ya Kitaifa ya siku mbili leo nchini Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu ziara hiyo Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amesema ziara hiyo ni matokeo ya kazi kubwa anayoifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na mataifa mengine.
“Ziara ya Mheshimiwa Widodo itakuwa ni ziara ya pili kwa kiongozi wa taifa hilo kutembelea nchini. Ziara ya kwanza ilifanywa Mheshimiwa Soeharto, Rais wa Pili wa Indonesia tarehe 05 Disemba 1991, miaka 32 iliyopita,” alisema Dkt. Tax.
“Mheshimiwa Rais Widodo atawasili tarehe 21 Agosti, 2023, na atapokelewa rasmi na Mwenyeji wake, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 22 Agosti, 2023, Ikulu Jijini Dar es Salaam,” aliongeza Waziri Tax.
Waziri Tax ameongeza kuwa, baada ya mapokezi viongozi hao watakuwa na mazungumzo ya faragha, na baadaye mazungumzo rasmi na kufuatiwa na hafla ya utiaji saini Hati za Makubaliano ya ushirikiano kwenye sekta mbalimbali.
@wizara_mambo_ya_nje_tz
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

