
TFS YATOA HEKTA 296,881 ZA MAENEO YA HIFADHI KWA WANANCHI KWA AJILI YA MAKAZI, KILIMO NA UFUGAJI
Kamishna wa Uhifadhi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)Prof. Dos Santos Silayo amesema amesema wakala umeendelea kutatua migogoro kati ya hifadhi za misitu na jamii inayoizunguka ambapo jumla ya hekta 296,881 za maeneo ya hifadhi zilitolewa kwa wananchi kwa ajili ya makazi, kilimo na ufugaji.
.
Silayo ameyasema alipokuwa akizungumza na aaandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya TFS na mwelekeo kwa mwaka wa fedha 2023/24 leo Agosti 16, 2023 katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.
.
Amesema kwa mwaka wa fedha uliopita, TFS ilizalisha jumla ya tani 25.9 za mbegu za miti na kuotesha miche 32,735,653 ya aina mbalimbali ambayo ilipandwa katika mashamba 24 ya Serikali na mingine kugawiwa kwa watu binafsi, taasisi na mashirika mbalimbali kwa ajili ya kupandwa katika maeneo yao.
.
"Hadi sasa, TFS imepanda miti katika hekta 6,909 na kurudishia miti iliyokufa kwenye hekta 2,434" amesema Silayo.
.
Silayo amesema kupitia filamu ya “Tanzania the Royal Tour”, TFS imejipanga kutumia fursa hiyo kuongeza tija katika uhifadhi, utalii na ukusanyaji maduhuli, ambapo juhudi zilizofanyika zimewezesha kuongezeka kwa idadi ya watalii waliotembelea vivutio vya utalii ikolojia ambapo hadi kufikia Juni 2023 jumla ya watalii 242,824 walitembelea vivutio hivyo.
.
"Idadi hii ni ongezeko la asilimia 60.8 ukilinganisha na watalii 152,002 waliotembelea vivutio hivyo kwa kipindi hicho kwa mwaka 2021.Jumla ya Shilingi 1,368,940,965 zilikusanywa ikilinganishwa na Shilingi 603,311,740 zilizokusanywa mwaka uliopita ikiwa ni ongezeko la Asilimia 12" amesema Silayo.
.
Kamishna huyo amesema katika eneo la ukusanyaji Maduhuli hadi kufikia Juni, 2023 jumla ya shilingi Bilioni 143.5 ambayo ni sawa na asilimia 96 ya makisio (projection) yote zilikusanywa na Kwa wastani kwa miaka miwili tumekusanya Jumla ya TZS 289.89 Bilioni Sawa na asilimia 102 ya makisio.
.
Aidha, Silayo amesema kwa mwaka jana 2022 wamefanikiwa kupunguza matukio ya moto katika misitu hapa nchini kwa asilimia 11%.
.
"ukiangalia mwaka uliopita tulikuwa na matukio mengi zaidi ambayo yalipelekea kupoteza takribani hekta 3200 kwenye misitu ya kupanda, mwaka tulipoteza kidogo takribani hekta 176" amesema.
#JordanMediaupdates
Tranding News

Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news