logo

MOLLY SIMS AJITOA KWA WATOTO NJITI, ACHANGIA SH.MILIONI 62.7

Mwanamitindo na Mwigizaji wa Kimataifa Molly Sims @mollybsims ambaye ni Mke wa Mwenyekiti wa Netflix Films, Scott Stuber, yupo nchini Tanzania ambapo August 12,2023 amechangia Dola Elfu 25 (Tsh. Mil 62.7) kwa ajili ya ujenzi wa wodi maalum ya Watoto wachanga wakiwemo Watoto njiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza.

Molly amechangia pesa hizo wakati akifungua kampeni ya ujenzi wa wodi hiyo katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba, wazo lililoanzishwa na Doris Mollel Foundation mwaka jana, ufunguzi huo umefanikishwa na Taasisi ya Kimataifa ya JHPIEGO na Doris Mollel Foundation, na kuhudhuriwa na Mkuu wa Idara ya Mama na Mtoto na Afya ya Uzazi wa Wizara ya Afya, Dkt. Felix Bundala pamoja na Viongozi kutoka Makao Makuu ya JHPIEGO Duniani.

Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel @dorismollel na Mkurugenzi Mkazi wa JHPIEGO Tanzania Alice Christensen kwa pamoja wameahidi kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo kushawishi Wadau wengine na Serikali kuchangia fedha nyingine za kumalizia jengo hilo.

Itakumbukwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alichangia pesa zake binafsi Tsh.Mil 70 kwa ajili ya kutoa hamasa ya ujenzi pamoja na kununua vifaa vya Watoto njiti katika Hospitali hio ya Wilaya ya Kwimba mwaka jana kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti Duniani yaliyoandaliwa na Doris Mollel Foundation.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn