ETHIOPIA YAANZA MSAKO WA WAPENZI WA JINSIA MOJA
Mamlaka za Ethiopia zimesema zimekuwa zikifanya msako katika hoteli, baa na maeneo ya burudani katika mji mkuu ambapo inadai vitendo vya mapenzi ya jinsia moja vinafanyika.
.
Ofisi ya Utawala wa Amani na Usalama ya Addis Ababa imesema ilikuwa ikichukua hatua "dhidi ya taasisi ambazo vitendo vya mapenzi ya jinsia moja vinatekelezwa".
.
Mamlaka ya jiji hilo ilisema hatua hiyo ilikuja baada ya taarifa kutoka kwa umma, na kusema kuwa tayari ilikuwa imevamia nyumba za wageni.
.
Imewataka wananchi kutoa taarifa kwa polisi kuhusu vitendo hivyo na kuongeza kuwa itaendelea na msako katika maeneo mengine.
.
Mapenzi ya jinsia moja ni marufuku nchini Ethiopia.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

