logo

HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA DODOMA YATENGEWA SHILINGI BILIONI 24

Mganga Mfawidhi Wa Hospitali Ya Mkoa Wa Dodoma Dkt.Ernest Ebenzi Amesema Kwa Mwaka 2023/24 Hospitali Hiyo imetengewa Shilingi Bilioni 24 ambapo Fedha Hizo zitaenda kukarabati na kujenga majengo kwa ajili ya kutolea huduma mbalimbali za afya.

.

Ebenzi Ameyasema Hayo Leo Agosti 09,2023 Alipokuwa akizungumza Na Waandishi Wa Habari Jijini Dodoma Kuhusu Utekelezaji Na Vipaumbele Vya Hospitali Hiyo Kwa Mwaka 2023/24.

Amesema Hospitali hiyo itaendelea kuwahudumia wananchi kwa wakati na huduma bora kwa gharama ndogo, kutumia muda mfupi katika kumuhudumia mgonjwa pamoja na uhakika wa dawa za kutosha.

"Hospitali Itaendelea kupiga hatua katika kutoa huduma bora kwa kuzingatia sayansi na teknolojia ya kisasa. Tunaendelea kufanya tafiti mbalimbali, kuwasomesha watumishi wa hospitali" Amesema Ebenzi.

.

Mganga Mfawidhi Huyo Amesema Kwa siku Hospitali ya Rufaa ya Dodoma inapokea wagonjwa zaidi ya 1,500 na hospitali ina uwezo wa kulaza wagonjwa 250 hadi 350 kwa wakati mmoja.

.

"Kwa kipindi cha mwaka mmoja yaani 2022/2023 Hospitali ilifanikiwa kufanya Kliniki tembezi katika maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Dodoma ambapo wagonjwa 552 walihudumiwa" Amesema.

.

Aidha, Ebenzi Amesema Wastani wa mahitaji ya damu kwa mwaka Hospitali Hiyo ni chupa/units 5,400, kipindi cha mwaka 2022/2023 chupa/Units 5,368 zilikusanywa sawa na asilimia 99% Na hakuna mteja aliyekosa damu.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn