AWESO AKUTANA NA MWIGULU NCHEMBA
WAZIRI wa Maji Mhe Jumaa Aweso amekutana na kufanya mazungumzo katika kikao kazi na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt.Mwigulu Nchemba.
.
Kikao hiki kilichohusisha makatibu wakuu na watendaji na wataalamu toka pande zote mbili yaani Wizara ya Maji na Wizara ya Fedha na Mipango kimefanyika Hazina Jijini Dodoma ambapo ajenda mbalimbali zimejadiliwa kwa lengo la kuongeza ufanisi katika Utekelezaji wa miradi ya Maji ambao unategemeana na upatikanaji wa fedha na zaidi kuweka mikakati itakayopelekea Mashirikiano mema kati ya sekta hizi mbili ili kufanikisha dhamira ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mwanamama ndoo kichwani.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

