MOI YATENGEWA SHILING BILIONI 55.9 KUBORESHA HUDUMA ZA TIBA NCHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo (MOI) Prof.Abel Makubi Amesema Vipaumbele Vya MOI Kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 Kwenda Kuanzisha Huduma Mpya Tatu za Kibingwa kibobezi ambazo Bado zinasababisha Rufaa Nje Ya Nchi( Tiba Ya Baadhi ya kiharusi Kupitia Angio- Suite, Tiba ya Baadhi ya Vifafa Kupitia Upasuaji na Upasuaji Wa kiuno Kwa Njia ya Matundu (Hip arthroscopy).
.
Makubi Ameyasema Hayo Leo Julai 03,2023 Alipokuwa akizungumza Na Waandishi Wa Habari akieleza utekelezaji wa majukumu ya Taasisi anayoisimamia ndani ya miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Sita na mipango ya Mwaka wa Fedha 2023/24 leo Agosti 3, 2023 kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.
.
Amesema Serikali imetenga Jumla ya Shilingi 55.9 Ili Kuboresha Huduma za tiba na Shughuli za Uendeshaji.
.
Mkurugenzi Huyo Amesema wamepanga Kuendelea kuwapa mafunzo wataalamu wao ili kuwaongezea ujuzi ambapo wataalamu 10 wanapelekwa kwenye mafunzo kupitia mfuko wa mafunzo wa Mama Samia na kuendelea kujengea uwezo watumishi wa Hospitali zingine za Kanda na Mikoa ili kupunguza mrundikano wa wagonjwa MOI na kutoa nafuu ya gharama kwa Wananchi.
.
Aidha, Makubi Amesema wataendelea kushirikiana na MUHAS, MNH, JKCI na Taasisi zingine katika kutoa Mafunzo na Tafiti katika eneo la Tiba ya Mifupa na Ubongo.
.
Naye Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg.Gerson Msigwa Amewataka Wananchi Kujenga utamaduni wa kwenda kupata matibabu hospitalini, Kwa Sababu Serikali imefanya mapinduzi makubwa katika kuimarisha huduma kwenye hospitali ya MOI na Nyinginezo nchini.
"Wananchi zitumieni, msikae na wagonjwa nyumbani na msiwapeleke wagonjwa tiba mbadala (waganga wa kienyeji), msisubiri wagonjwa wazidiwe na kuwapeleka wagonjwa hospitali wakiwa wameshafika katika hali mbaya" Amesema Msigwa.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

