BMH HOSPITALI YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KUTOA HUDUMA YA UPANDIKIZAJI WA UROTO
Mkurugenzi Mtendaji Wa Hospitali Ya Benjamin Mkapa (BMH) Dkt.Alponce B.Chandika Amesema Hospitali hiyo Ndio Ya Kwanza Pekee Katika Ukanda Wa Afrika Mashariki ambayo imewezesha kuanza Kutoa Huduma Ya Upandikizaji Wa Uroto Kwa Wagonjwa hapa Nchini.
.
Chandika Ameyasema Hayo Leo Agosti 01,2023 Alipokuwa akizungumza Na Waandishi Wa Habari Kuhusu Utekelezaji Wa Majukumu ya Hospitali Hiyo Na Mwelekeo wake Kwa Mwaka Wa Fedha 2023/24 Katika Ukumbi Wa Habari Maelezo Jijini Dodoma.
.
Amesema Huduma hiyo inasaidia Watoto Wagonjwa Wenye matatizo la Selimundu(Sickle Cell) hivyo uanzishwaji Wa Huduma hiyo Umekuwa mkombozi Kwa Wagonjwa kwa Tanzania na Nchi zinazoizunguka.
.
"Tangu kuzinduliwa kwake Huduma Hizi tumeshahudumia Watoto 4 Kwa Tanzania Na Gharama Yake kwa wastani, Mtoto Mmoja zinagharimu Takribani Milioni 50-70. Kama kutibiwa Nje Ya Nchi Gharama Yake kwa Mtoto Mmoja Milioni 120-135" Amesema Chandika.
.
Mkurugenzi Huyo Amesema Kwa mwaka huu wa fedha 2023/24 Serikali imewatengea Bilioni 64.52 katika hizo Shilingi Bilioni 18.6 zinakwenda kwenye miradi ya maendeleo ili kuendelea kuwapunguzia wananchi adha ya kusafiri mbali kupata matibabu.
.
"Maendeleo hayo ni kuendeleza ujenzi wa jengo la saratani ambao mpaka sasa umefikia asilimia 27, hivyo kwa kutengewa pesa hizi zitasogeza zaidi ujenzi" Amesema Chandika.
.
Aidha, Chandika Amesema Eneo lingine ni ujenzi wa jengo la matibabu ya moyo na kifua kwa watoto na watu wa zima(Cardiovascular and Thoracic Center), wanatarajia kuanza ujenzi huo mwaka huu wa fedha nayo ni katika lengo la kuwapunguzia adha wananchi kusafiri mbali kupata matibabu.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

