logo

WAZIRI MKUU MAJALIWA AONGOZA NBC DODOMA MARATHON

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa @kassim_m_majaliwa ameongoza wananchi mbalimbali katika Mbio za NBC Dodoma Marathon zilizofanyika leo Julai 23, 2023 Jijini hapo.

Akizungumza mara baada ya mbio hizo Mhe. Majaliwa ameipongeza Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kuanzisha mbio hizo, ambazo zina lengo la kusaidia kuboresha afya ya Mama na Mtoto ambapo amesema takriban Shilingi Milioni 500 zimekusanywa.

Kwa upande wake Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Sekta ya Michezo ni nyenzo muhimu ya kuleta mabadiliko katika afya ya jamii, kwakua kwa kushiriki michezo na mazoezi idadi ya magonjwa yasioambukiza inapungua, huku akiiasa Mikoa na Halmashauri nchini kuendelea kutenga na kujenga miondombinu ya michezo.

Mbio hizo ambazo baadhi ya Watumishi wa wizara hiyo wameshiriki, zimeshirikisha KM 5, 10, 21 na 42 kwa Wanaume na Wanawake ambapo washindi wamepata zawadi ya fedha taslim na medali.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn