logo

PPRA YAWATAKA WATUMISHI WA UMMA,WAZABUNI KUZINGATIA MAADILI KATIKA UTENDAJI WAO

WITO umetolewa Kwa wanaojihusisha Na Ununuzi Wa Umma Ikiwemo Watumishi Wa Umma na Wazabuni Kuzingatia Maadili Katika Utendaji wao na Kufuata taratibu Na Kanuni zinazoongoza Eneo Hilo la Ununuzi Wa Umma.

.

Wito Huo umetolewa Na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw.Eliakim Maswi Alipokuwa Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Juu ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2023/24 leo Julai 17, 2023 kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.

.

Maswi Amesema Mamlaka hiyo haitosita kuwachukulia Hatua Kwa Mujibu Wa Sheria wale Wote watakaokiuka Utaratibu au Watajihusisha Uovu Wowote utakaoisababisha Serikali Hasara.

.

Amesema Tangu Julai 1, 2023 Mfumo wa NeST umeanza kutumika rasmi hivyo Taasisi Nunuzi zote ikiwa ni pamoja na Wizara, Idara za Serikali, Taasisi zinazosimamiwa na Msajili wa Hazina na Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, zinapaswa kuanza kutumia Mfumo mpya kwa shughuli za Ununuzi wa Umma kuanzia Mwaka wa Fedha 2023/24.

.

"Vilevile, ununuzi wa bidhaa na huduma mtambuka na ununuzi unaofadhiliwa na wadau wa maendeleo ambao wanatumia nyaraka zao za zabuni, utaendelea kutumia mfumo wa TANePS hadi Septemba 30, 2023, baada ya tarehe hiyo tunaamini Taasisi zote zitakuwa zimepata mafunzo ya Mfumo mpya" Amesema Maswi.

.

Aidha, Maswi Ujenzi wa Mfumo mpya wa ununuzi kwa njia ya mtandao ujulikanao kama “National e-Procurement System of Tanzania (NeST)”, una lengo la kuhakikisha Ununuzi wa Umma nchini unazingatia kuongeza uwazi kwenye Ununuzi wa Umma, usimamizi mzuri wa fedha za umma, kudhibiti vitendo vya rushwa na ufuatiliaji wa ukidhi wa sheria, uwajibikaji na udhibiti wa ununuzi.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn