logo

WAZIRI UMMY AWATAKA WANANCHI KUWAFICHUA WATUMISHI WANAOFANYA VITENDO VIOVU HOSPITALINI

WAZIRI wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu Ametoa wito kwa wananchi wote Nchini kuibua Vitendo Vibaya vinavyofanywa Na Baadhi ya Watumishi wa Afya katika vituo vya kutoa huduma za Afya vya umma na binafsi ili kuongeza uwajibikaji katika Utoaji wa Huduma za Afya nchini kwa kuwa Afya zetu ni wajibu wetu.

.

Ummy Ameyasema Hayo Leo Julai 8,2023 Mara Baada Ya Kuiona Video Fupi iliyosambaa Mtandaoni ikimuonesha Mtumishi wa Afya akichambua, kusafisha na kuanika vifaa vya Hospitali katika Hospitali ya Kivule Mkoani Dar es Salaam.

.

Amesema Kitendo hicho ni kinyume na taratibu na miongozo ya Kanuni za Udhibiti wa Maambukizi (Infection Prevention and Control).

.

"Tayari Viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam wanalifanyia kazi suala hili na watatoa Taarifa Rasmi. Ninamshukuru mwananchi aliyerekodi na kuisambaza clip hii" Amesema Ummy.

.

Aidha, Ummy Ametoa Rai kwa wataalamu wa afya kuzingatia mafunzo na mihiko ya kazi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

.

"Wizara ya Afya kwa kushirikiana na OR Tamisemi tutaendelea kuchukua hatua ili kuimarisha ubora wa huduma" Amesema.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn