logo

JKT YAJITOA KUISAIDIA JAMII KATIKA UCHANGIAJI WA DAMU

MKUU Wa Huduma za Sheria Makao Makuu Ya Jeshi La Kujenga Taifa (JKT) Kanali Projest Christopher Rutaihwa Ameitaka Jamii na Wananchi Wote Kwa Ujumla Kujitokeza Kwa Wingi Katika Zoezi la Uchangiaji Damu linaloendeshwa Na Jeshi Hilo Ili kuokoa Maisha Ya Watu Wengine Wenye uhitaji Wa Damu Hospitalini.

.

Kanali Rutaihwa Ameyasema Hayo Leo Julai 7,2023 (Akimwakilisha Mkuu Wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele) Alipokuwa Akiongoza Zoezi la Uchangiaji Damu linalofanyika Kwa Siku 2 (Leo Na Kesho) Katika Viwanja Vya SUMA JKT House Jijini Dodoma.

.

Amesema Zoezi Hilo linalofanyika Leo linaendelea Katika Vikosi vingine Vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Nchini Kwa Sababu Lengo ni Kuokoa Maisha Ya Watu Wenye uhitaji Wa Damu.

.

"Leo Tuko Hapa Kwa Ajili ya Watu Wa Dodoma, Maafisa Na Askari Pamoja Na Vijana wote watafika Kwa Ajili Ya Zoezi hili, Lakini Pia Kwa Watu waliopo Katika Mkoa Wa Dodoma tunawakaribisha Sana Katika Zoezi Hili.

.

"Zoezi hili Ni Muhimu, Wahitaji Wa Damu ni wengi Mno Lakini kama Hautahitaji Damu Leo Ipo Siku ambayo na Wewe utahitaji Damu. kwahiyo ni Zoezi ambalo Tunahamasisha Jamii Nzima iwe inashiriki zoezi kama Hili. Na Sio la Siku Moja Tu linatakiwa liwe Endelevu" Amesema Rutaihwa.

.

Kanali Rutaihwa Amesema Jamii inapaswa ihamasishwe ijue Katika Kuchangia Damu Ni Harakati za kuokoa Maisha Na Pia Kuwasaidia wale Ambao ni Wahitaji Wa Damu Kwa Sababu Mahitaji Ni Makubwa Sana.

.

Aidha, Kanali Rutaihwa Amesema JKT kama Mdau Na Mshiriki Muhimu Katika Jamii ya Kitanzania linaonesha Zoezi Hilo Kwa Mfano Kwamba wapo Bega Kwa Bega Na Serikali Katika Kuchangia Damu.

.

Kwa Upande Wake Mkuu Wa Kitengo Cha Damu Salama Kutoka Hospitali Ya Benjamin Mkapa Dodoma, Mtekinolojia Wa Maabara Bw.Cos Michael Kibaja Amesema Ametoa Rai Kwa Watanzania wengine Kujitokeza Kwa Wingi Katika Zoezi Hilo na Kuchangia Damu Pamoja na Kutembelea Ofisi za Damu Salama Ili kuweza Kuchangia Damu.

.

"Unapoteza Dakika 10 Hadi 15 Kuchangia Chupa 1 ya Damu ambayo Ina Uwezo Wa kuokoa Maisha Ya Watoto 2 mpaka 3, Tuendelee Kuchangia Damu Ili Tuweze kuokoa Maisha Ya Watu" Amesema Kibaja.

.

Tukio Hilo limefanyika ni Katika Kuelekea Maadhimisho Ya Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambapo Kilele Chake Ni Julai 10,2023.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn