logo

DKT.MPANGO AZINDUA TAWI JIPYA LA NMB BANK BUHIGWE MKOANI KIGOMA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango Jana Julai 04,2023 Amezindua Rasmi tawi la Benki Ya NMB Buhigwe Mkoani Kigoma Ili kuweza Kuwasaidia wakazi wa hapo na maeneo jirani kunufaika na huduma zote za kifedha ikiwemo kufungua akaunti, kuweka na kutoa pesa, mikopo, kubadilisha fedha za kigeni, huduma za bima pamoja na ushauri wa masuala ya kifedha na biashara.

.

Tawi hilo linafanya NMB Kuwa na jumla ya matawi 229 nchi nzima, huku wakiendelea kuwafikia Watanzania kwa ukaribu zaidi.

.

Kwa Upande Mwingine, Uzinduzi Huo ulienda sambamba na kuigusa jamii ya sehemu hiyo ambapo Benki Ya NMB imekabidhi msaada wenye thamani ya jumla ya Shilingi Milioni 82.4 unaojumuisha, Vitanda vya ngazi (Double Decker) 100 kwa ajili ya shule ya sekondari Kahimba, Mabati 192 kwaajili ya Shule ya Msingi Nyamiti, Mabenchi 10 ya kukalia wagonjwa kwa ajili ya Zahanati ya Kasumo.

.

Vitanda vya ngazi (Double Decker) 100 kwaajili ya Shule ya Sekondari Nyumbikwa, Mabati 192 kwaajili ya Shule ya Msingi Kalema, Vitanda vya ngazi na Magodoro yake (Double Decker) 50 kwaajili ya Shule ya Sekondari Kasumo.

.

Msaada huo umepokelewa na Makamu wa Rais Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango aliyeambatana na CGF (Rtd).Thobias Andengenye ambaye Ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NMB Dkt.Edwin Mhede, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi,na viongozi wengine wa Serikali kwa niaba ya wananchi wa Buhigwe na maeneo jirani.

@nmbtanzania

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn