JKT YASHIRIKI USAFI NA KUTOA MSAADA HOSPITALI YA CHAMWINO,DODOMA
KUELEKEA Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa, Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii wa Jeshi la Kujenga Taifa, Kanali Regina Matina, kwa niaba ya Mkuu wa JKT, ameongoza zoezi la kufanya usafi katika Mazingira ya Kituo cha Afya Chamwino, Jijini Dodoma.
Kanali Matina ameyasema hayo katika Kituo cha afya Chamwino, wakati wa zoezi la kufanya usafi kwenye hospitali hiyo linaloenda sambamba na utoaji zawadi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi la Kujenga Taifa, ambayo kilele chake itakuwa Julai 10, 2023.
"Ni vizuri jamii ikazingatia makuzi na malezi ya mtoto,na moja ya vitu vya kuzingatia na kumpeleka Kliniki mtoto ambapo huko utapata elimu ya lishe bora kwa mtoto kutoka kwa wataalam wa Afya," alisema Kanali Matina.
Akizungumzia tukio hilo Kanali Matina, alisema ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi hilo tangu lianzishwe, pamoja na kuunga mkono jitihada za serikali za kutunza mazingira, aidha katika tukio hilo, Zawadi zilizotolewa kwa wagonjwa waliolazwa Kituoni hapo ni Pempasi pamoja na sabuni.
Naye Katibu wa Kituo cha Afya cha Halmashauri ya Chamwino, Bw.John Daniel amelishukuru Jeshi Hilo Kwa msaada walioutoa kwa wagonjwa pamoja na kufanya usafi wa mazingira jambo ambalo limeonyesha jamii kwamba Jeshi hilo lipo karibu na Wananchi.
Kwa upande wake Bi.Arafa Kombe ambaye amelazwa Kituoni hapo, ameishukuru JKT kwa kuwapa zawadi mbalimbali, Na kuwa tendo hilo linadhihirisha kuwa Jeshi la Kujenga Taifa kupitia kwa Maafisa, Askari, Vijana pamoja na Watumishi wake, wanajali Utu wa raia.
@wizara_ya_ulinzi
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

