PPRA YATAMBULISHA MFUMO MPYA WA UNUNUZI WA UMMA KIELETRONIKI(NeST)
RAI imetolewa Kwa Watanzania wote Hasa Wazabuni Kupokea Mfumo Mpya Wa Ununuzi Kwa Njia Ya Mtandao (NeST) utakaoleta Mageuzi makubwa Katika Ununuzi Wa Umma Kwa Kuanza Kujisajili Katika Mfumo Ili kuondoa usumbufu pale Mfumo utakapoanza Kutumia kwa Taasisi nunuzi zote.
.
Hayo Yamesemwa Na Mwenyekiti Wa Bodi Ya Wakurugenzi Ya Mamlaka Ya Udhibiti Wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Dkt.Leonada R.Mwagike Leo Juni 23,2023 Jijini Dodoma Alipokuwa Akizungumza Na Waandishi Wa Habari.
.
Mwagike Amesema Mfumo Huo utakwenda Kupunguza Mianya ya Rushwa Kwani Kumekuwa na Wazabuni Ambao Hawana Vigezo na Kupelekea Kusababisha Rushwa mara Kwa mara.
.
"Mojawapo Ya Sababu Ya Rushwa Ni Uwepo Wa Wazabuni Ambao Hawana Vigezo, Mfumo Uliopo Sasa Unaotoa mwanya Kwa Wazabuni kushawishi Maamuzi ya Vyombo Husika kama Bila vitengo Vya Manunuzi, Bodi za Zabuni Na Maafisa Masuhuli" Amesema Mwagike.
.
Mwenyekiti Huyo Amesema Baadhi Ya Taasisi ambazo zimeshaanza Kutumia Mfumo Huo Rasmi kama Sehemu ya Majaribio ni TANROADS na TARURA ambapo Zabuni Kutoka Taasisi hizo zimeshaanza Kutangazwa.
.
Amesema Taasisi Nunuzi Zote hazitaruhusiwa Kuendesha Michakato ya Ununuzi Nje Ya Mfumo Wa NeST Kuanzia Tarehe 01 Mwezi Oktoba,2023.
.
Aidha, Mwagike Amesema PPRA Itaendelea Kupokea Maoni Ya Wadau Mbalimbali Ili kuendelea Kuboresha Mfumo Huo Kwa kadri ya Mahitaji mapya, Na Kwa hivi Sasa Mfumo Huo unapatikana Katika Tovuti Ya www.nest.go.tz.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

