logo

CHONGOLO ATAKA MRADI WA KILIMO (BBT) UKAMILIKE MWEZI AGOSTI MWAKA HUU

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg.Daniel Chongolo ameiagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha miradi ya kilimo kwa vijana (BBT) inaanza kufanya kazi ifikapo mwezi Agosti mwaka huu.

Chongolo amesema miradi hiyo inatakiwa ikamilike haraka ili matokeo yaliyo kusudiwa yaanze kuonekana hususani kwa kundi lililokusudiwa la vijana.

Ndugu Chongolo amesema hayo katika leo Jumamosi, Juni 17, 2023, wakati akiwa siku ya tatu ya ziara yake akipita kusikiliza changamoto za wananchi, kuhamasisha uhai wa Chama na kukagua utekelezaji wa wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Mkoa wa Dodoma, alipofika kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Bwawa la Msagali, wilayani Mpwapwa.

Katika hatua nyingine, Chongolo amewataka wataalamu kukaa kwenye miradi hadi ikamilike ili kama kuna changamoto zitakazojitokeza wawajibike moja kwa moja.

Amesisitiza kuwa uwekezaji wa wataalamu katika maeneo ya miradi uende sambamba na kuonekana kwa matokeo chanya katika miradi ya maendeleo.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM ameongoza na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema na Katibu wa NEC-Oganaizesheni Issa Hajji Gavu.

@ccmtanzania

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn