logo

WAZIRI NDUMBARO APIGA MARUFUKU KUTOA MIKOPO BILA MWENZA KUJUA

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Mhe. Dk. Damas Ndumbaro (Mb) ameziagiza Taasisi za mikopo (microfinance) kuhakikisha mwenza wa anayempa mkopo nae amesaini ili kuondoa migogoro katika familia.

Waziri Huyo aliyasema hayo jana mkoani Shinyanga wakati akitoa elimu pamoja na kutatua migogoro mbalimbali ya kisheria kwa wananchi wa Maganzo, wilayani Kishapu ikiwa ni siku ya tano ya kampeni inayoendelea ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia iliyolenga kutoa elimu na msaada wa kisheria bure kwa wananchi hasa wa vijijini ambao hawawezi kumudu gharama za mawakili.

Ndumbaro alisema kuwa kumekuwa na ongezeko la migogoro katika familia kufuatia mmoja wa wanandoa kuchukua mkopo bila mwenza wake kujua hali inayopelekea kuchukuliwa kwa thamani za nyumbani au hata nyumba kuuzwa pindi mkopo huo unaposhindwa kurejeshwa.

“Kwa mujibu wa sheria ya ndoa. Wewe ambae unatoa mkopo lazima uhakikishe mwenza wa huyo unayempa mkopo nae amesaini.Ukimpa mke peke yake mume hajui, au ukampa mkopo mume peke yake bila mkewe kujua imekula kwako.

"Na ukiona taasisi hiyo iliyomkopesha mwenza wako bila wewe kujua na kusaini una haki ya kukataa wasizuie au kuuza mali ya familia,” alisema Ndumbaro.

@katibanasheria_

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn