RAIS MSTAAFU KIKWETE MGENI RASMI 'JKT MARATHON 2023'
RAIS Mstaafu wa Awamu Ya Nne Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa Kuwa Mgeni Rasmi katika Mbio za JKT 2023 (JKT MARATHON 2023) zinazotarajiwa kutimua vumbi Juni 25,2023 Katika Uwanja Wa Jamhuri Jijini Dodoma.
.
Hayo Yamesemwa Na Mkurugenzi Wa Elimu,Michezo Na Utamaduni Makao Makuu Ya Jeshi La Kujenga Taifa (JKT) Kanali Erasmus Bwegoge Alipokuwa akizungumza Na Waandishi Wa Habari Makao Makuu Ya Jeshi Hilo Chamwino Jijini Dodoma kuhusiana na Mbio hizo kuelekea miaka 60 ya JKT tangu kuanzishwa kwake.
.
Kanali Bwegoge Amesema JKT linatarajia Kutimiza Miaka 60 Tangu kuasisiwa Kwake Ifikapo Tarehe 10 Mwezi Julai 2023 na Jeshi Hilo limepanga Kufanya Shughuli Mbalimbali Ikiwemo Mashindano Ya Mbio yanayojulikana kama 'JKT MARATHON 2023'.
.
"Mbio Hizo zitafanyika Juni 25,2023 na Zitafanyikia Jijini Dodoma ambapo zitaanzia na kumalizikia Uwanja Wa Jamhuri ambapo Mgeni Rasmi atakuwa RAIS Mstaafu wa Awamu Ya Nne Mhe.Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
.
"Mbio Hizi zitakuwa Na kilomita Tofauti aina 3; Zitakuwepo Mbio za Kilomita 5, 10 na kilomita 21.1 zote zitaanzia Uwanja Wa Jamhuri na Kumalizikia Uwanja Wa Jamhuri" Alisema Bwegoge.
.
Aidha, Amesema Mbio za Kilomita 5 zitaanzia Uwanja Wa Jamhuri- Barabara ya Iringa - Milembe- Nyerere na Kurejea Uwanja Wa Jamhuri, Na Mbio za Kilomita 10 zitaanzia Uwanja Wa Jamhuri (Kupitia Barabara ya Iringa), Kupitia St.John Round About- Barabara ya Kikwete - Barabara Ya Hazina, Barabara ya Veta, Barabara ya Dar es Salaam Kurudi Barabara ya Nyerere, Barabara ya Jamhuri Na Kumalizikia Uwanja Wa Jamhuri.
.
Amesema Mbio Hizo zitaanza Rasmi Kwa Ratiba iliyopangwa Saa 12:10 Asubuhi ambapo wakimbiaji Wa Kilomita 21.1 wataanza, Na Saa 12:20 watafuatiwa na Wakimbiaji watakaoshiriki Mbio Za Kilomita 10, Na itakapofika Saa 12:30 Mgeni Rasmi Mhe. Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete atawasili na Yeye Atashiriki Kukimbia Mbio za Kilomita 5 ambazo zitaanza Saa 12:40.
.
"Tunategemea Mbio Hizi Kuwa zimekamilika Ifikapo Saa 6:00 Mchana, na Baada ya Mbio Hizo kutakuwa na Matukio Mengine ya Utoaji Wa Zawadi, Shamra Shamra na Burudani zingine ambazo zitakuwa zimeandaliwa Kwa Mujibu Wa Ratiba" Alisema Mkurugenzi Huyo.
.
Aidha, Bwegoge Amesema Mbio Hizo zitawashirikisha Wananchi Wote na Wanakaribishwa Kwa Hivi Sasa Kuendelea Kujiandikisha Kwa Ajili Ya Mashindano.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

