'MPISHI WA NIGERIA' HILDA BACI AVUNJA REKODI YA KUPIKA
Juhudi za mpishi wa Nigeria kuvunja rekodi ya kupika kwa muda mrefu bila kukoma zimetambuliwa rasmi na Guinness World Records (GWR).
-
Hilda Baci alianza kuvuma nchini humo baada ya kupika kwa siku nne mwezi uliopita.
-
Alipika kwa saa 100 na aliruhusiwa mapumziko ya dakika tano kila saa.
-
Hata hivyo GWR imeweka rekodi yake kwa saa 93 na dakika 11, na kupunguza muda wa saa saba kwa alizochukua mapumziko.
-
Hilda anaipiku rekodi ya hapo awali kwa zaidi ya saa tano iliyowekwa huko Rewa, India 2019 na mpishi wa India Lata Tondon aliyepika kwa saa 87 dakika 45.
#JordanMediaupdates
Frank Jordan
12345
123
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

