
RAIS SAMIA AWATAKA WAKULIMA KUACHA KUUZA MAZAO NJE YA NCHI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Amewataka wakulima wote Nchini kutokuuza Mazao Nje ya Nchi na Badala Yake wasubirie Serikali iweze Kununua Mazao Hayo Hapo Baadae.
.
"Msiuze mazao nje ya nchi, tusubiri Serikali inunue mazao hayo.Natoa rai kwa wakulima kutunza chakula cha kutosha kwa ajili ya familia zao" Amesema Samia.
.
Samia Ameyasema Hayo Leo Juni 13,2023 Wakati wa Ufunguzi wa Tamasha la Bulabo lililoandaliwa na Kituo Cha Utamaduni Wa Wasukuma Bujora lililofanyika Mkoani Mwanza.
.
Amesema Mwaka huu 2023 itatolewa Fedha ya kununua chakula hivyo Kama Nchi tunataka kuwa na hifadhi ya tani 500,000 kwenye maghala yetu.
.
Kwa Upande mwingine Rais Samia Amewaomba Machifu wote nchini kusaidia katika malezi, kusimamia mila, desturi na tamaduni katika maeneo yetu na kuhakikisha vijana wanaelewa umuhimu kwa kuenzi utamaduni wa Taifa na kuwa na maadili mema kwani vijana bila usimamizi Taifa litapotea.
.
Naye Waziri wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Mhe.Balozi Dkt.Pindi Chana Ametoa Rai kwa vikundi vyote vya Sanaa na Wasanii Binafsi Hapa Nchini kuhakikisha wanafanya usajili Kwa kutumia njia ya mtandao kupitia tovuti www.sanaa.go.tz.
.
Aidha, Chana Amewasihi wazazi na walezi kuwalea na kuwakuza watoto na vijana wao katika misingi ya maadili ya utamaduni wa Mtanzania.
#JordanMediaupdates
Tranding News

Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news