
TRA YATAKIWA KUTOKUKUBALI KUSAFIRISHA WALA KUINGIZA BIDHAA BANDIA NCHINI
WAZIRI wa Uwekezaji, Viwanda Na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji Ameitaka Mamlaka Ya Mapato Tanzania (TRA) kutokukubali Kusafirisha na kuingiza Bidhaa Bandia Nchini, na Pia kutokukubali Kusafirisha na kuingiza Wakala Wa Ushuru Wa Forodha Ambao wapo Chini Ya Mamlaka Hiyo.
.
"Uwepo Wetu Kwenye Mipaka Ni Muhimu Sana na Ni Rahisi Kuzuia zikiwa Mipakani kuliko kuzitafuta zikisha Ingia Ndani ya Soko La Taifa Letu Ni Ngumu Mno" Amesema Kijaji.
.
Kijaji Ameyasema Hayo Alipokuwa Akifungua Kongamano la Maadhimisho Ya Siku Ya Udhibiti Wa Bidhaa Bandia Duniani 2023 Leo Juni 13,2023 Jijini Dodoma Katika Ukumbi Wa Mabele.
.
Amewataka Watumishi Wa Tume Ya Ushindani kuchukua Hatua Kali za Kinidhamu pale Ambapo watakapogundua Mtumishi Yeyote yule wa Tume Hiyo ambaye amejimilikisha Alama ya Muwekezaji, Mzalishaji kwenda Kwa Mtu ambaye anataka Kutengeneza Bidhaa inayofanana na Hiyo.
.
Waziri Huyo Amesema Katika Miezi 9 ya Mwanzo ya Mwaka Wa Fedha 2022/23 Tume hiyo ilikagua Makasha Ya Kusafishia Mizigo 7,918 Katika Bandari Ya Dar es Salaam ambapo Kati Ya Hayo Makasha 206 Tu Sawa Na Asilimia 2.6 yalikutwa yakiwa Na Shehena ya Bidhaa zinazokiuka Sheria Ya Alama za Bidhaa.
.
"Hii inamaanisha Asilimia 97.4 Ya Bidhaa zilizoingia na zilizokaguliwa Ndani ya Taifa Letu zote zilikidhi Matakwa ya Alama za Bidhaa. Kwa Takwimu Hii zinaonyesha Wazi Kuwa Tume Ya Ushindani Kwa Kushirikiana na Vyombo Vingine Vya Serikali, na Waingizaji Pamoja na Wazalishaji wa Bidhaa Mbalimbali mnafanya Kazi Nzuri Lakini Bado. Hii Asilimia 2.6 inatuambia Tupo kwenye Hatari" Alisema Kijaji.
.
Kijaji Amesema Ni Muhimu Watumishi hao Kuendelea Kuifanya Kazi Yao Vizuri na Endapo wakilegeza Kidogo Tu itaongozeka Zaidi, hivyo waendelee Kusimamia na Kushirikiana.
.
Aidha, Kijaji Amewataka Watumishi hao Kuendelea Kutoa Elimu Kwa Ushirikiano Kwa Sababu Tume Ya Ushindani Peke Yake Hawawezi Kwa Sababu Kuna Vitu Pia Hawana hivyo Lazima Ushirikiano Uwepo.
#JordanMediaupdates
Tranding News

Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news