CRDB YATUNUKIWA TUZO YA 'BENKI BORA AFRIKA MASHARIKI'
BENKI ya CRDB imetunukiwa tuzo ya Benki Bora ukanda wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2023 katika tuzo zilizotolewa na Jarida la African Banker zilizofanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB).
Tuzo hiyo inatambua mageuzi makubwa ambayo Benki hiyo imeyafanya katika biashara yake na ambavyo yamesaidia katika kutengeneza thamani endelevu, kuongeza ujumuishi wa kifedha, na kujenga ujumuishi wa kiuchumi kupitia bidhaa, huduma, na mifumo bunifu ya kidijitali.
Tuzo hiyo ya ‘Benki Bora Afrika Mashariki’ ni mwendelezo wa benki ya CRDB kutambuliwa kwa ubora kimataifa ambapo mwaka jana ilitunukiwa tuzo mbili za ‘Benki Bora Tanzania’ na Jarida la Euromoney’ la Uingereza na ‘Global Finance’ la Marekani.
Katika Mkutano Mkuu wa AfDB, CRDB kupitia Meneja Mwandamizi wa Ubia na Ushirikiano wa Kimkakati, Masele Msita ilishiriki mdahalo wa African Banker Live uliozungumzia jitihada za mabenki barani Afrika kuziwezesha biashara zinazomilikiwa na kuongozwa na wanawake sambamba na programu ya AFAWA.
@crdbbankplc
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

