SAGINI AWATAKA WANA BUTIAMA KUFICHUA TAARIFA ZA WAHALIFU WASHUGHULIKIWE
NAIBU Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama Mhe. Jumanne Sagini amewataka Wananchi wa Mkoa wa Mara Wilaya ya Butiama kuhakikisha kuwa wanatoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kutoa taarifa za siri kwa wale wote wanaoshiriki katika matukio mbalimbali ya kihalifu ili waweze kubainika, kuchukuliwa hatua za Kisheria.
Sagini ameyasema hayo Mei 31,2023 wakati akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mmazami Kata ya Bukabwa na Wananchi wa Kijiji cha Mwibagi Kata ya Kyanyari Wilayani Butiama kufuatia kuripotiwa kwa vitendo vya kihalifu vilivyoanza kushamiri katika siku za karibuni katika Wilaya Hiyo yakiwemo mauaji, kujeruhiwa kwa vijana 8 wanaoshiriki katika ulinzi shirikishi na matukio ya wizi.
“Serikali imesikitishwa sana na matukio ya takribani wiki mbili yaliyotokea katika Wilaya ya Butiama.Ninawapa pole sana kwa niaba ya Serikali kwa wote mliokumbwa na changamoto hiyo.
.
"Faraja yangu ni kwamba kwa Wananchi wote mliozungumza hapa hakuna aliyetayari kuona Wananchi ambao wamejitahidi kujitafutia mali zao wanakuja kudhurumiwa na watu ambao ni wavivu, hawajiangaishi na kufikiri wanaweza kujinyanyua kiuchumi kwa kupora mali za wenzao, hilo halikubaliki kwa vyovyote vile" Alisema Sagini.
.
Naibu Waziri Huyo Amesema IGP Wambura amefanya mabadiliko ya Viongozi wa Kipolisi katika Mkoa wa Mara na ameleta Makamishna wawili kutoka Polisi Makao makuu, Na wote walioletewa katika Mkoa huo wapo kazini hivyo amewaomba waamini kwamba Wahalifu wote waliofanya uhalifu Mmazami na Vitongoji vyake watapatikana Tu.
Aidha, Sagini Amewataka wazazi Kuunga Mkono Kipindi ambacho wahalifu hao watakapokuwa wanashughulikiwa.
.
"Nataka niwaambie mtu anaanza kujifunza kuiba akiwa nyumbani mnaponyamaza na kuwatetea hasa Wakinamama mnafanya makosa. Madhara yake akizoea uhalifu anakwenda kuiba kwa mwingine”Alisema Sagini.
Naye Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi CP Awadhi Haji amesema kuwa kwa matukio yote yaliyokwisha kutokea hatua kali zimeanza kuchukuliwa na Jeshi hilo.
@wizaramnn
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

