MWANAMKE MWENYE MIAKA 19 BRAZIL AJIFUNGUA MAPACHA WENYE BABA TOFAUTI
Mwanamke mwenye umri wa miaka 19 nchini Brazil ameripotiwa kujifungua mapacha ambao kila mmoja ana baba tofauti wa kibaolojia, hali ambayo imethibitishwa kupitia vipimo vya DNA.
.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwanamke huyo alifanya tendo la ndoa na wanaume wawili katika siku moja, na baadaye akabeba mimba ya mapacha.
.
Vipimo vya DNA vilibaini kuwa kila mtoto alirithi vinasaba kutoka kwa mwanaume tofauti.
.
Hali hiyo inajulikana kitaalamu kama heteropaternal superfecundation, ambapo mayai mawili yanayotolewa katika mzunguko mmoja wa hedhi kurutubishwa na mbegu za kiume kutoka kwa wanaume wawili tofauti.
Tukio hilo ni nadra sana na limeripotiwa kutokea katika visa vichache duniani.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

