logo

ULEGA:SERIKALI YAONGEZA USALAMA BARABARANI KWA KUFUNGA TAA NCHINI ‎

Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi Bungeni jijini Dodoma leo Jumatano Mei 20, 2026 , ameeleza namna serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inavyoweka kipaumbele katika usalama wa watumiaji wa barabara kwa kufunga taa za barabarani.

‎Katika simulizi ya kipekee, Waziri Ulega amekumbusha tukio lililotokea KigongoBusisi katika daraja la JP Magufuli, ambapo kwa mara ya kwanza taa za barabarani zilipowashwa, mkazi mmoja wa kutoka ukabila la Wasukuma alilala nje ya nyumba yake akidhani bado ni mchana na usiku bado haujaingia.

‎Tukio hilo limekuwa kielelezo cha mabadiliko makubwa yanayoletwa na uwekaji wa taa za barabarani, hatua inayoongeza usalama na kuonyesha dhamira ya serikali kuimarisha miundombinu ya usafiri nchini.

‎Serikali imesisitiza kuwa uwekaji wa taa za barabarani ni sehemu ya mkakati mpana wa kuhakikisha usalama wa wananchi na kuondoa changamoto za ajali na hatari za usiku barabarani na kuwezesha biashara kufanyika nyakati zote usiku na mchana.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn