logo

WATOTO WA SELIMUNDU KUNUFAIKA NA MFUKO MPYA WA MATIBABU WA BMH ‎

Menejimenti ya Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imebuni mfuko wa kushirikisha wadau (stakeholders) kuwezesha kusaidia matibabu ya Upandikizaji wa Viungo kwa kuanza na Upandikizaji Uloto kwa watoto wenye Selimundu(Sickle cell) na Upandikizaji Figo kwa Wananchi wenye Uhitaji.

‎Akiwasilisha mpango huo kwenye mkutano wa Wenyeviti wa Bodi na Wakurugenzi wa Mashirika ambayo Serikali ina hisa ndogo (Miinority Interest Forum ) ulioandaliwa na ofisi ya Msajili wa Hazina, mjini Arusha, Mkurugenzi Mtendaji wa BMH ,Prof.Abel Makubi ameeleza kuwa mfuko huo unajengwa kwa Dhana ya Wadau wenye Moyo wa Huruma wa kusaidia huduma za matibabu zenye gharama kubwa kwa Wananchi wenye uhitaji katika kuunga mkono juhudi za Serikali.

Prof. Abel Makubi ameeleza kuwa mfuko huo unachangiwa na wadau kutoka mashirika ya umma chini ya uratibu ya Msajili wa Hazina,Mashirika Binafisi na mtu mmoja mmoja, na unategemewa kukusanya shilingi Bilioni 7 ndani ya miaka miwili ili kusaidia huduma hizo katika Matibabu, vifaa, kupanua miundombinu mbinu na kuendelea kujengea uwezo watalamu wa taaluma hizo.

Mfuko huo unategemewa kuzinduliwa rasmi tarehe 8 Mei 2026 katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 10 ya BMH, na Wadau takribani 200 wameshirikishwa katika mpango huu.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn