MUIGIZAJI MICHAEL B. JORDAN AANDIKA HISTORIA MPYA HOLLYWOOD 2026
Muigizaji maarufu wa Marekani Michael B. Jordan ameandika historia mpya katika tuzo za Academy Awards baada ya kushinda tuzo ya Best Actor, ikiwa ni mara ya kwanza kwake kutwaa tuzo hiyo kubwa katika taaluma yake ya uigizaji.
.
Ushindi huo unamuweka Jordan katika kundi dogo la waigizaji Weusi waliowahi kushinda tuzo hiyo muhimu katika historia ya Hollywood.
.
Safari ya mafanikio ya Jordan imejengwa kupitia filamu kadhaa zilizompa umaarufu mkubwa, zikiwemo Fruitvale Station, Creed na Black Panther.
.
Kupitia kazi hizo, ameendelea kuthibitisha kipaji chake na kuwa mmoja wa waigizaji wenye ushawishi mkubwa katika Hollywood ya kisasa.
.
Ushindi wake katika filamu Sinners umeongeza hatua nyingine muhimu katika historia ya kazi yake, huku mashabiki na wadau wa tasnia ya filamu wakimpongeza kwa mafanikio hayo makubwa.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

