BARABARA YA TENGERU HADI MIRERANI KILOMITA 28 KUWEKWA KIWANGO CHA LAMI
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuanza ujenzi wa barabara ya Tengeru- Mirerani km 28 kwa kiwango cha lami.
Dkt.Nchemba ameyasema hayo leo Februari 22,2026 alipokuwa kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa hostel za wanafunzi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela mkoani Arusha .
Nae Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema Wizara ya ujenzi itahakikisha Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), inaweka wakandarasi watatu ili barabara hiyo ikamilike mapema na itumike kwenye michuano ya AFCON 2027.
"Kukamilika kwa barabara hiyo kutaongeza barabara mbadala za lami na kupunguza msongamano jijini Arusha", amesisitiza Eng. Kasekenya.
Naibu Waziri Kasekenya amesema barabara za jiji la Arusha zitawekwa taa na kupambwa na mabango ya kuelezea michuano hiyo ya AFCON 2027.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

