DKT.MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA CHUO KIKUU MZUMBE,KAMPASI YA TANGA
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 15, 2026 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa miundombinu ya Chuo Kikuu Mzumbe kampasi ya Tanga ambayo hadi kukamilika kwake kutagharimu zaidi cha shilingi bilioni 12
Chuo hicho kinachojengwa katika kata ya Gombero, Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, unatekelezwa kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi” (“Higher Education for Economic Transformation” – HEET”)
Miradi inayoendelea kutekelezwa kupitia mpango huo ni Ujenzi wa Jengo la Taaluma lenye jumla ya madarasa 6, Maktaba ndogo, Ukumbi wa mihadhara, maabara mbili zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kila moja, pamoja na ofisi 36 zitakazohudumia wafanyakazi 72.
Aidha, Majengo mengine ni Hosteli 2 za wanafunzi, Bwalo la Chakula, Kituo cha afya kitakachohudumia wanafunzi, wafanyakazi na wananchi wa vijiji vilivyopo jirani na Chuo, Nyumba 4 za Wafanyakazi, Mfumo ya majitaka na dampo la kuhifadhia taka ngumu pamoja na Tenki la kuhifadhi Maji Safi la ujazo wa lita laki 4.
Hadi kufikia Februari 13, 2026 ujenzi wa kampasi hiyo ulikuwa umefikia asilimia 82.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

