WATATU WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA KWA KUSAFIRISHA MIRUNGI
Mahakama ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, ikiongozwa na Hakimu Mkazi Mkuu Mhe. Kimaro, imewahukumu kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja washtakiwa watatu baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi.
Mshtakiwa wa kwanza, Debora Mwita Marwa, alipatikana na hatia ya kusafirisha mirungi yenye uzito wa kilogramu 25.5, huku mshtakiwa wa pili, Jackline Chacha Mwita, akihukumiwa kwa kusafirisha kilogramu 13.3 za dawa hiyo.
.
Katika shtaka jingine, Debora Mwita Marwa pia alikutwa na hatia ya kusafirisha bunda 24 za mirungi.
Mahakama ilibainisha kuwa makosa hayo ni kinyume na Kifungu cha 16(1)(2)(a) cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Sura ya 95 (Marejeo ya mwaka 2023).
.
Washtakiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti na maafisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

