logo

SIMULIZI YA MAMA MAGRETH MWIBULE YAHITAJI MSAADA WA WATANZANIA

Mwaka 2023, Mwandishi wa Habari Bw. Frank Jordan akiwa pamoja na Mtangazaji Dkt. Isaac Maro, walifanya mahojiano maalum kupitia kipindi cha NJIAPANDA kinachorushwa na Redio ya Clouds FM kila Jumapili.

‎.

‎Mahojiano hayo yalihusisha Mama Magreth Mwibule, mjane na mkazi wa Mtaa wa Sokoine,Chamwino Jijini Dodoma.

‎Mama Magreth kwa hivi sasa ni mlemavu wa miguu yote miwili, hali iliyotokana na ajali ya gari aliyoipata mwaka 2012 katika eneo la Hombolo, Jijini Dodoma.

‎.

‎Tangu wakati huo, ameshindwa kabisa kusimama au kutembea, jambo lililobadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.

‎Licha ya ulemavu huo, Mama Magreth ana jukumu kubwa la kulea watoto wake wawili wa kiume peke yake baada ya kufiwa na mume wake miaka kadhaa iliyopita.

‎.

‎Mtoto wake wa kwanza anatarajiwa kumaliza elimu ya Kidato cha Sita (Form Six) mwaka huu, huku mtoto wa pili akimaliza Kidato cha Nne mwaka jana 2025.

‎Hata hivyo, hali ya afya ya Mama Magreth bado ni tete, hususani kutokana na maumivu na matatizo ya mguu wake wa kulia, hali inayomfanya ashindwe kujihudumia ipasavyo.

‎.

‎Kutokana na mazingira magumu ya maisha anayopitia, anahitaji msaada wa Watanzania wenye moyo wa kujitolea ili aweze kupata huduma muhimu za kijamii ikiwemo matibabu, mahitaji ya msingi ya nyumbani pamoja na msaada wa maisha ya kila siku.

‎Kwa yeyote ambaye Mungu amemjalia na yuko tayari kumsaidia, anaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mama Magreth Mwibule au kuchangia kupitia namba ya simu 0654-576150 (Jina: MAGRETH MWIBULE).

Mchango wowote, mdogo au mkubwa, ni faraja na tumaini jipya kwa Mama Magreth na watoto wake.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn