ALIYEBAKA WATOTO YATIMA SABA AHUKUMIWA MAISHA JELA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Januari 08, 2026 imemhukumu Stephano Anyosisye Mwasala (35), mkazi wa Msongola, kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuanzisha kituo cha kulelea watoto bila leseni pamoja na kubaka na kuwanyanyasa kingono watoto saba waliokuwa chini ya uangalizi wake.
Mwasala alikuwa mmiliki wa kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu kiitwacho Majest Children Home, kilichopo Msongola, Kibaha.
Mahakama ilibaini kuwa kati ya Desemba 2024 na Januari 2025, mshtakiwa aliwafanyia vitendo vya kingono watoto hao wenye umri kati ya miaka 10 hadi 14.
Upande wa Jamhuri ulieleza kuwa baada ya kupokea taarifa hizo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa Ustawi wa Jamii walimkamata mtuhumiwa, kufanya uchunguzi na kisha kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma zilizomkabili.
Akisoma hukumu, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mhe. Joyce Mkhoi amesema mshtakiwa amekiuka Sheria ya Mtoto Sura ya 13 ya mwaka 2019 kwa kuanzisha kituo bila leseni, pamoja na Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 (Marejeo ya 2022) kwa makosa ya ubakaji.
Mahakama amesema adhabu hiyo ni fundisho kwa wengine na kulinda watoto dhidi ya ukatili.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

